Saturday, August 30, 2008

Will Smith akutana na Rais wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar mh. Amani Abeid Karume akiongea na mcheza sinema wa Marekani Will Smith
Rais wa zanzibar mh. Amani Abeid Karume na mkewe Mama Shadya katika picha ya pamoja na Will Smith na mai waifu wake Jada Pinkett Smith leo huko Ikulu, Zanzibar.
Picha kwa hisani ya kwa mdau Othman Maulidi wa Zanzibar.

1 comment:

Mzanzibar 100% said...

zanzibar ni njema, atakae aje! Ukija zanzibar utapelekwa ikulu kama Willy...!

Halafu utapata wenyeji wenye ukarimu na upendo, watakutembeza dole, mchamba wima, mnara wa mbao, soko muhogo, na malindi pia utapelekwa ukaone simba na ukali wake alivyonyweshwa chai..! Ha ha ha usiogope, kama utashindwa kukaa kwenye MKEKA utapewa KIGODA ukalie!Zanzibar MINAZI tele, kuna mirefu na mifupi (twaita kitamli), minene na myembamba! Kama utapenda kula nyama ya dafu ukisha kunywa maji yake basi UTACHOKOLEWA, na ukinunuwa vocha ya simu pia UTASUGULIWA wala hupati tabu Zenji raha kila kitu wafanyiwa..!
Na kama WALI WA KUNDE ukisha iva UTAPAKULIWA (zanzibar hakuna self service), yaani kila kitu we utakarimiwa! Kama huna kazi mashaallah..utapelekwa pwani ya KIWENGWA ukapare samaki au "UTAPARA MIWA" mahonda! Huko mahonda ndo kwenye kiwanda chetu cha sukari, zanzibar miwa teleeeeeeeeeeeee!