Thursday, August 14, 2008

Michango Inahitajika - Marehemu Jacob Castory Mpogole


Michango bado inahitajika kusafirisha mwili wa marehemu -Jacob Castory Mpogole

Ndugu WATANZANIA mwili wa marehemu Jacob Castory Mpogole sasa upo tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Tanzania na mipango imeshafanywa ya kuusafirisha mwili mwisho wa Juma hili.Familia ya marehemu inashukuru kwa michango ambayo imetolewa hadi sasa ambayo kwa tathmini za mpaka jana usiku zilikuwa zimefikia £1300, lakini bado tunahitaji michango zaidi ili kuweza kufanikisha kusafirisha mwili wa marehemu katika muda uliopangwa, hivyo Watanzania wote na marafiki wa Tanzania mnaombwa kusaidi kuchangia chochote kile ili kufanikisha zoezi hili la kupeleka mwili wa marehemu katika sehemu yake ya mapumziko.Kikao cha mwisho kitafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 Agosti 2008.

Bank: LLOYDS TSB
Account Name: Mrs. Ummy H. Shella
Account Sort Code:77-91-09
Account Number:13923068
Kassim-07985488194
Ummy-07962338257
Abubakar Faraji
Swift Freights Uk Ltd.
Unit 62-8 Fountayne Road
London N15 4QL
United Kingdom
Tel:0208-801-9800
Mobile -07852260024

*****************************************************************

Thursday, 7 August 2008

MTANZANIA AFARIKI LONDON
Polisi mjini London wana mwili unaosadikika kuwa wa Bwana Jacob Castory Mpogole, mwili wa marehemu upo mikononi kwa Polisi na jitihada zinafanyika kutafuta ndugu jamaa na marafiki ili watambue mwili wa marehemu.

Kama wewe ni ndugu jamaa au rafiki wa Jacob Castory Mpogole unaombwa uwasiliane na Ubalozi wa Tanzania 0207-569-1470 au Tanzania Association -0208-801-9800

****************************************************
JUMUIYA YA WATANZANIA INAOMBA MICHANGO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU JACOB CA MPOGOLE
Ndugu wa marehemu Jacob Castory Mpogole wamepatikana na siku ya Jumamosi kilifanyika kikao nyumbani kwa Kassim na Ummy katika maeneo ya Stockwell, London kuhusiana na utaratibu wa kufanya ili kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu.
Watanzania wengi walijitokeza na kuchangia kwa hali na mali katika jitihada za kuchangia gharama za kusafirisha mwili wa marehemu Jacob.

Jumuiya ya Watanzania inawaomba watanzania na marafiki wote wa Tanzania kusaidia katika kuchangia gharama za kusafirisha mwili wa marehemu kwa kuwasiliana na Bwana Kassim katika namba au kuweka pesa katika akaunti iliyopo hapa chini.

3 comments:

Anonymous said...

Jamani, huu utaratibu wa kurudisha maiti nyumbani naona kama unazidi kuwa mgumu, na zaidi kama unategemea michango ya watu.....kama marehemu hakuwa na insurance au salio lolote bank kwa nini isipendekezwe azikwe tu hukuhuku? Mchango upelekwe kwa familia iliyokuwa inamtegemea.

Anonymous said...

Jamani Castro yamekukuta yapi tena jamaniii.....RIP my dear.
Da Chemi mbona leo blog yako imenitokea puani mwenzenu.
Please kwani yalimkuta yapi tena??...ndugu zake wa karibu niliokuwa nawasikia mdomoni wake ni huyu aliyekuwa waziri Mr. Mungai na Danny Mpogole ambaye ni meneja mkuu MUFINDI COMMUNITY BANK (MUCOBA).....Halafu,,,Castro...au utaratibu wa kuunganisha kazi bila kupumzika ndio uliokuponza jamani??.....sina ninachokielewa...Castro ulikuwa mtu mzuri sana jamani.....Pumzika kwa amani dear......Jamani basi Da chemi tuelezeni basi huku Tz msiba uko wapi jamani....Kapumzike kwa amani baba........RIP

Anonymous said...

Si wachome moto maiti. ndugu yake akisafiri kwenda Bongo anatia majivu kwenye hand luggage. akifika Bongo anazimina kwenye ardhi huko kijijini kwake. Twendeni na wakati mabo ya kusafarisha maiti yamepitwa na wakati.