Thursday, August 21, 2008

Kulikuwa hakuna Makuu!

Rais Kikwete akihutubia Bunge leo

Imeandikwa na Beda Msimbe

Gumzo la lukwangule:Nilichovuna saa 4 za kumsikiliza rais

JANA nilisema kwamba kutakuwa na makubwa leo. Naamini saa nne za kumsikiliza JK hazikuzaa hasara kama mtuma habari. Lakini kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi yapo makubwa yaliyoainishwa na kutolewa ufumbuzi ambao unaweza usiwe bora leo lakini miaka kadhaa ijayo.

Jambo la msingi ambalo mimi nimeliona ni kuwa masulaa niliyodhani atayagusa aliyagusa, sikutarajia mengi makubwa katika EPA kwa kuzingatia mfumo wa sheria wa nchi yetu, lakini kwa sasa wabunge waliokuwa hawaelewi nini EPA sasa watakuwa wameelewa.

Nilichotoa hai katika EPA ni kufilisiwa kwa watu, kunyimwa nafasi ya kusafiri na fedha hizo zinazorejeshwa kusaidia wakulima kwa kuanzisha ruzuku katika mbolea na pia katika kusaidia TIB yaani Tanzania Investment Bank kuwa na uwezo wa kukopesha wakulima kwa muda nrefu na riba nafuu.

Swali linalobaki je hawa wahuni waliotwaa fedha ambazo si za serikali lakini serikali inaweza kudaiwa watafanywa nini? Matajiri azimio la Arusha walishughulikiwa kwa kurejesha mali zao kwa umma je hawa hawastahili kweli kushtakiwa, wanasheria wanajua lakini la maana zaidi utawala wa sheria hauna maana ya kuachia wakwivi kutokomea hivi hivi tu lakini pia si kwa kuwafanya waingie mahakamani bila kigezo, hawa ni wevi au wajanja hilo ni swali kwanza kisha... waswahili wanasema habari ndio hiyo... lakini amesema kwamba Novemba Mosi kitaeleweka mahakamani.

Nilisema shauri la Zanzibar lakini kidiplomasia kabisa kasema watu wasikoroge mambo na kwamba ukiwa nje ni tanzania ukirejea hapa unazungumza zanzibar, alitumia akili sana kuhusu hili hasa aliposema wimbi hili nalo litapita walio watu wazima wasiwe wapuuzi, nadhani kimeeleweka.

Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Bunge hilo kwa mara ya pili tangu ashike madaraka mwishoni mwa mwaka 2005 nilichoona kama alivyowahi kusema katika hotuba yake ya kwanza alitumai tena fursa hiyo kuelezea mwelekeo wa uchumi wa taifa na masuala mbalimbali ambayo serikali yake imekuwa ikiyapa kipaumbele.

Na shida zote alisema tusigombee fito, tunajenga nyumba moja na hili siwezi kulikataa, lakini inakuwaje unapokuwa na watu ambao hawaelewi hasa nini wanatakiwa kukifanya, na watu hao wakiwa viongozi? Lipo tatizo la ufinyu wa sheria na utawala pengine Sitta yuko sahihi sheria zetu zinaruhusu mambo kuenenda kigoigoi zaidi.

Huu muungano nao aliuzungumzia vyema, alisema wazi ubaya wa uropokaji, alisema matamshi ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya viongozi yanaweza kuchangia kuwavuruga kama siyo kuwachochea wananchi.

Ilivyo ni kwamba kama ni kujadili suala la Muungano basi hapana budi mjadala ufanyike kwa hekima na busara na siyo jazba kama ambavyo imejitokeza katika siku za karibuni, hili siliendelezi sana.Na huu mpasuko wa Zenj kumbe ulishafikia hatua nzuri lakini jamaa hawa wa Unguja kama wanavyosema katika suala la U nchi na Usio nchi amesema wanashindwa kuaminiana.

Kitu ambacho nilikiona kuwa kidogo cha mgomo, kumbe sivyo, rais alizungumzia haki ya watu kugoma, lakini ndani ya sheria, ndani ya uelekezi wa kawaida uliokubalika, kama kweli ni mgomo unaostahiki. Hapa alifafanua vyema kuhusu mgomo unaokuja, hakuugusia wa walimu lakini huu wa TUCTA alisema mpaka kwa Kiingereza haukubaliki. Alikuwa na vigezo vyake.Alisema kwamba mfuko wa hazina baada ya makubaliano sio ATM ni lazima kuweka sawa baada ya bajeti na walizungumzia Agosti sasa watu watazame kama serikali haitalipa.

Kweli kabisa serikali kwa mgao wa kota si ATM lakini nini maana ya maneno yote hayo ambayo serikali inazungumza. Inamaananisha kwamba haipo tayari kuyumbishwa, makubaliano ni muhimu watu wa TUCTA wanajua wamevumilia kiasi gani lakini wachambuzi wa mambo wa naweza pia kuelewa kwa kina nini maana ya kauli ya serikali kuhusiana na njia zilizotumika kutangaza mgomo.

Shauri la mwisho ambalo mimi nilisema ni la kawaida ni matumizi mabaya ya uhuru wa kunadika na kusema, maandamano,kupiga domo, kupinga serikali,kushughulikia hasira na kutuliza munkari.kwa haraka haraka unaona kwamba alikuwa anachimba mkwara, lakini kama yeye aliwezesha upana wa mambo katika kucheua sumu mwilini alitaka watu wawe wastaarabu wasitapike bila mpangilio wakawavushia matapishi wenzao wakabaki wananuka bila sababu.

Hili halina ubishi kucheua sumu muhimu lakini utapike kwa mipangilio na uwe na sababu sio uachie tu mradi mdomo wa kutapikia unaoKimsingi mimi nasema rais saa zake nne hazikuwa mbaya sana ingawa haya mengine ni elekezi za kawaida za nini amefanikisha katika miaka miwili na miezi saba ya utawala wake, kilichobaki ni kuangalia ushauri wa spika kwamba kunahitajika kasi zaidi kushughulikia wanaohujumu uchumi kwa mtindo wa EPA.

Naam, kweli tunahitaji mabadiliko kwani hii ni salamu, kazi yenyewe bado iko kwa wananchi wenyewe, ni hotuba inayotakiwa kuchambuliwa, kuna mengi sana ambayo sikuyatia hapa kwani huenda yakasaidia miaka mitatu ijayo wakati wa uchaguzi: ni ukweli kuwa wanaobungua nchi hii ni viongozi wafanyabiashara kwa hiyo tunahitaji waamue ama kuwa na biashara au kuwa wanasiasa na viongozi, hata ughaibuni linajulikana.

4 comments:

Anonymous said...

Work Done = Zero

Anonymous said...

Ha ha ha swadkta anon wa kwanza, au kwa lugha ya ki mathematics tunasema niswawa na Quadratic equatio!!!

Anonymous said...

Mheshimiwa Rais JK atunukiwe digrii ya uzamivu (Ph.D) ya usanii!!
Watuhumiwa wa wizi - iwe ni mali ya serikali (wananchi) au watu binafsi - huwa wanapelekwa mahakamani kujibu tuhuma!!

Anonymous said...

Naoan wezi Wa EPA waliundiwa kamati ya Makasisi MAPDRE wkaungama na kisha labda katika masharti ya malipizi ni kurudisha PESA, mmojawapo wa Padre Ni Rais Kikwete, ndiyo maana majina yao yanatunzwa kutokana na siri ya Maungamo, haa haa msanii Kikwete, ndanagaya toto Bagamoyo lakini hii Ni Tanznia sasa. tupo 2010:KALABAGAO NA UBWEZI WAKE>>>>>