Friday, August 08, 2008

Tanzia - Mama Ethro Yohane Gadau

(Marehemu Mama Ethro Gadau)
Taarifa ya msiba

Habari za leo ndugu wanajumuiya,

Alfajiri ya leo tumepokea taarifa ya msiba wa mama yetu mpendwa Ethro Yohane Gadau. Mama Ethro amefariki dunia asubuhi ya leo tarehe 7 August 2008 katika hospitali ya West Houston Medical Center iliyopo hapa Houston kutokana na “shinikizo la damu” lililompata tarehe 5 August 2008.

Marehemu Ethro alizaliwa tarehe 12 Decemba mwaka 1956. Marehemu, alikuja Houston miezi miwili iliyopita kumtunza mwanae, Jane Wella, na mjukuu wake mchanga, Naomi Mbuyah.. Ameacha mume (Eleutherius J. Wella), watoto wanne (Pamella, Andrew, Jane, na Clara), na wajukuu wawili – Labron Wella, na Naomi Mbuyah.Kikao cha awali cha maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu mama yetu kwenda Dar-es-Salaam, Tanzania kimefanyika leo jioni 7 August 2008 nyumbani kwa Jonas Mbuya.

Kikao hiki kilichoongozwa na Mzee Leonard Tenende kimechagua viongozi wa msiba huu kama ifuatavyo:M/Kiti: Mathew Mohono 281 804 6478M/Hazina: Jonas Mbuya 832 428 5621Wasemaji wa msiba huu: Ephraim Mpendaamani na DominoWanakamati: Nuru Mazola,Lilian Maliti,Toni Makinda, Margareth Jenga, Mami Kasomi na Mariam Janguo.

Pia kikao hiki kwa pamoja kimeamua kuwa na harambee siku ya Jumamosi tarehe 9 August 2008 kuanzia saa kumi kamili jioni (4pm) (ukumbi bado unashughulikiwa na tutawajulisha mara tu tukipata taarifa). Mipango ya sehemu ya kuhifadhia mwili wa marehemu bado inashughulikiwa na Bw. Juma Maswanya.

Juhudi zinafanyika ili hiyo sehemu tuweze kuitumia kuaga mwili wa marehemu siku ya Jumapili(August 10).Makadirio ya usafirishaji wa mwili ni dola elfu kumi na nane ($18,000.00). Makadirio haya yanahusisha gharama zote za kuufikisha mwili wa mama yetu mpendwa nyumbani Tanzania.

Kwa sababu hiyo basi, kwa niaba ya familia ya Mzee Wella wanajumuiya tunaombwa tujitolee kwa kadri ya uwezo wetu ili tuweze kufanikisha lengo letu la $18000. Wanajumuiya tunaombwa tuwe na kiwango cha chini cha dola mia($100) kama rambirambi. Pia kama una chochote ambacho ungependa kutoa kwa ajili ya mnada tafadhali wasiliana na yeyote hapo juu.

Pia kwa kurahisisha shughuli hii akaunti imefunguliwa kwa ajili ya wale walio nje ya jiji la Houston. Benki ni WACHOVIA. Routing Number: 111015159 Akaunti namba ni: 1010199794410.

Waliopo kwenye akaunti hii ni JONAS MBUYA na ANDREW WELLATumfariji Jane – mwanajumuia mwenzetu – pamoja na familia yake katika kipindi hiki kigumu sana cha kumpoteza mama yetu mpenzi.

Anwani ya nyumbani kwake ni:
2751 Wallingford Dr. #2912
Houston, TX 77042….. Gate code 2369

Tunaomba akina mama/dada walete vyakula na akina kaka/baba walete vinywaji wanapokuja msibani na siku ya harambee.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Amina

EPHRAIM MPENDAAMANI
Msemaji wa Msiba (kwa niaba)

No comments: