Tuesday, October 28, 2008

Dar es Salaam kumezwa na bahari


Imaandikwa na Maura Mwingira, New York

JIJI la Dar es salaam ni kati ya miji mikuu 19 Barani Afrika ambayo imo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na uongezeko la kina cha maji ya bahari kunakosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Hayo yamo katika ripoti ya mwaka 2008/09 ya hali ya miji mikuu duniani (State of the World’s Cities), taarifa ambayo imeziduliwa mbele ya waandishi wa habari, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, (UN- HABITAT) Bibi Anna Tibaijuka.

Ripoti hiyo ambayo hutolewa kila miaka miwili inaonya kuwa ni miji mikuu michache sana iliyoko katika ukanda wa bahari itakayonusurika na janga hilo.

Pamoja na Dar e s salaam, miji mikuu mingine ambayo imo katika hatari ya hiyo na hata kutoweka kabisa ni pamoja na Abijani, Accra, Alexandria, Algiers, Capetown, Casabalanca, Dakar, Djibout, Durban, Freetown, Lagos, Libreville, Lome, Luanda, Maputo, Mombasa, Port Louis na Tunis.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa UN-Habitat, Anna Tibaijuka, anatoa wito kwa serikali zote kutoa kipaumbele katika kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na tishio hilo lilodhahiri la mabadiliko ya yali ya hewa.

Anasema serikali za mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea yote yanakabiliwa na hatari hyo, hivyo zinatakiwa kuzingatia masuala ya mipango miji endelevu na inayoweka mbele maslahi ya watu maskini ambao ndio watakaoathirika zaidi kutokana na athati hizo za kuharibiwa kwa mazingira na ongezeko la joto duniani.

Taarifa hiyo inafafanua na kubainisha kwamba si muda muda dunia itaanza kushuhudia madhira ya mabadiliko ya hali ya hewa , na hasa katika wakati huu ambao zaidi ya asilimi 50 ya watu wanaishi katika miji.

Na kwamba hali itakuwa mbaya zaidi kwa afrika kwa kuwa haina mipango mkakati madhubuti ya kukabiliana na majanga ya kibinadamu na hasa yale yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Taarifa hii ambayo walengwa wake ni waandaaji wa sera na wahusika wa mipango miji, pamoja na mambo mengine inalenga kutoa tahathari kwa kuonyesha ni miji mikuu ipi ambayo katika hatari kubwa ya kuathirika na ongezeko la kina cha maji na ni jumuia zipi zinazoweza kutoweka kabisa katika uso wa dunia.

Kwa mujibu wa taarifsa hiyo, katika karne iliyopita ya 20, ilikadiriwa kuwa kina cha maji kiliongezeka kwa sentimeta 17, na kwamba inatarajiwa kuwa kati ya mwaka 1990 hadi 2080 kina cha maji kitaongezeka kati ya sentimeta 22 na 34.

Aidha taarifa hiyo , inaeleza zaidi kwamba kuna miji mikuu3,351 ulimwenguni ambayo aidha iko yako chini ya usawa wa bahari, au haiku mbali sana na usawa wa bahari, na kwamba asilimia 64 ya miji hiyo iko katika nchi zinazoendelea.

Huku Asia ikiwa na zaidi ya nusu ya miji mikuu hiyo na ambayo yako katika hatari kubwa, ikifuatiwa na Bara la Amerika na Caribbean lenye asilimia 27 ya Miji Mikuu, na Afrika ikiwa na silimia 15.

Aidha Bara la Ulaya lina robo tatu ya miji mikuu, huku moja ya tano ya miji yote katika America ya Magharibi iko chini ya usawa wa bahari.Pamoja na kuonesha ni miji mikuu ipi itakayoathiriwa na ongezeko hilo la kina cha maji, taarifa hiyo pia inaelezea hali halisi ya ukuaji wa miji mikuu, idadi ya watu inaoingia katika miji hiyo, hali ya huduma za jamii , lakini pia inaainisha utofauti wa makazi uliopo kati ya watu matajiri, wa kipato cha wastani na maskini kabisa.

Aidha ripoti hiyo inaonyesha kwamba katika kila watu watatu katika nchi zinazoendelea, mmoja anaishi katika makazi duni (slums) Taarifa hiyo pia inabainisha kwamba karibu watu milioni tatu kila siku wanaingika katika miji mikuu na miji hususani katika nchi zinazoendelea.

Inaonyesha taarifa hiyo kwamba ifikapo kati kati ya karne ya 21 idadi ya watu wanaoishi katika miji mikuu katika nchi zinazoendelea itaongezeka maradufu kutoka watu bilioni 2.3 mwaka 2005 hadi bilioni 5.3 ifikapo mwaka 2050 Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bara la frika na kama hali hii ya watu kukimbili kuishi katika majiji na miji mikubwaitaendelea, basi ifikapo mwaka 2050 idadi ya kubwa ya watu wake itakuwa inaishi katika miji mikubwa, huku kukiwa na watu 1.2 bilioni watakaokuwa wakiishi katika majiji na miji hali itakyoifanya afrika kuwa na robo ya watu wote duniani wanaoishi katika miji mikuu.

Mwisho.

2 comments:

Anonymous said...

Ah, Kumbe jiji letu la Dizim linapendeza hivi...!! Itakuwa simanzi kubwa likimezwa na bahari.

Anonymous said...

KWAKO DADA CHEMI TUNAITEGEMEA SANA BLOG YAKO KUTUPA KINACHO AJILI KILA SAA,DAKIKA,SEKUNDE KINACHO ENDELEA NA UCHAGUZI WA UKO KWENU KWA JINSI ULIVYO BOBEA TUNAAMINI UTATUPA LATEST EVERY SECOND SASA INAKUJE AU BADO UMELALA?USHINDI WA ONYANGO NI UKOMBOZI WA MWAFRIKA LETE HABARI USITUBANIE LOV,MDAU CARDIFF