Monday, August 18, 2008

Watumwa


Wadau, ukienda Bagamoyo kutalii lazima utaonyeshwa 'Fort' amabako watumwa walipelekwa kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kabla ya kwenda Arabuni. Huko waliambiwa "bwaga moyo".

Nimeona hi picha ya watumwa na baadhi ya waarabu waliokuwa wanawauza.

7 comments:

Anonymous said...

chemi watumwa hawakuwa wakipelekwa uarabuni. soma historia ujuwe waikuwa wakipelekwa ulaya na marekani. nenda nchi yoyote leo hii ya uarabuni kama utakuta athari zozote za kuwepo vizazi vya watumwa. waarabu walikuwa wanafanya biashara ya kuuza watu lakini wateja wao ni ulaya na marekani sio kupeleka uarabuni. kule ulaya na marekani walikuwa wanalimishwa mashamba. baada ya mapinduzi ya viwanda wakawa wanatumikishwa katika viwanda hasa katika kuprocess malighafi.uarabuni hakuna kitu hakuna mashamba wala hakukuwa na viwanda. wao wenyewe waarabu walihamia maeneo mbali mbali ya dunia kwa ajili ya kutafuta maisha bora sasa hao watumwa wa kazi gani kwao. kwahiyo napenda ujuwe kuwa wauzaji walikuwa waarabu na wateja walikuwa wazungu. wote kundi moja hawa hakuna aliye mwema hapa.

Anonymous said...

Waafrika walipelekwa arabuni. Wanaume walikuwa castrated (kukatwa mboo). Wanawake walitumiwa kwa aji ya ngono. Watoto wao walihesabiwa kama waarabu na ni sababu huoni weusi wengi huko Arabuni. Unaona waarabu waliochanganya damu wengi.

Anonymous said...

watumwa wote waliotoka east coast of africa walipelekwa arabuni,kutoka west coast ndio walipelekwa new world

Anonymous said...

huyo anony wa 1 alikimbia umande kwakweli.

Anonymous said...

Anon wa juu kabisa umekosea. Hawa watu walikuwa wanawahasi kama anon wa pili aliyesema na kama ikitokea unazaa mtoto alikuwa anauwawa. Sasa mimi huwa najaribu kujiuliza, utumwa uliwa hivi miaka ya karibuni na dini zote mbili zimekuja miaka dahali, dini zikuwa wapi kukemea hiyo biashara na mauaji? Hawa wote ni wauaji tu, kwanza mtu anapingana mambo ya dini wakati ni mwafrika namdharau sana. Sasa vita yao ni mafuta sio Uislam na Ukristo

Anonymous said...

huyo anonim wa hapo juu namwunga nkono
kwa kweli nimekuwa nafikiri sana juu ya dini na waaarabu na wazungu
mwafrika kabla wazungu na waarabu kuja huku tulikuwa hatujui mohamad wala yesu
wao ndio walileta hiyo dini kwa waafrika na siyo waafrika waliwapelekea dini waarabu na wazungu atleast kwa mujibu wa nyaraka za kihistoria zilizoweza patikana unless kama kuna ushahidi tofauti unaopatikana juu ya hili suala
lakini mpaka sasa kwa mujibu wa ushahid wa kihistoria unaonyesha kwamba mzungu na mwarabu ndiye aliyeleta dini kwa mtu mweusi
na kwamba ushahidi unaonyesha kwamba waafrika walikuwa na dini zao fulani kabla ya kuja hawa jama
sasa basi inanishangaza na kuniuma saana ninaposikia mwafrika anamwua mwafrika mwenzie eti kisa ni dini! ili hali zile zetu wenyewe tumezitupa pia inanikera kuona waafrika tunatengana kwa sababu ya dini aidha uislamu au ukristo ili hali kabala ya kuja hao walizileta tulikuwa tuna utanzania wetu ,walitukuta na utanzania wetu na wala si uislamu au ukristo lakini leo hii kizazi hiki kipo tayari kumtenga mtu mwingine sababu ya dini na hali dini yenyewe si yake ni mapokeo tu
kwa kweli sioni matiki hapa na ukweli ni kwamba dini hizi tunazojidai nazo zililetwa hapa kwetu kwa mtutu wa bunduku na upanga nina maana huku wanatupa dini na at the sametime wanatuchukua utumwa
inashangaza sana kuona mtu mweusi akipapatikia uislamu au ukristo utadhani wao ndio wenye dini ukiangalia lifestyle ya wazungu na ile ya waarabu na hasa ukiangalia uovu (udhambi) ulioambatana na maisha yao halafu uje kwa watanzania kweli unaweza kusema waafrika ni malaika !
dini zoote mbili hizi zimetuua na kututesa sana waafrika na hata wazungu wenyewe walikufa saana kwa dini(angalia historia ya kanisa katoliki inatisha!) na kisha angalia historia ya uislamu (mambo ya kusarenda) teba! inatisha na histiria ya dini zoote mbili hizi imeghubikwa na damu ,ushenzi,udhambi wa kila aina ktk jina la yesu na mohammad

Anonymous said...

warabu walinunuwa kwa waswahili kwanza ndio na wao wakauza ukumbuke kwanza kulikuwa na madalali ambao wakiwapelekea hao watumwa warabu