Tuesday, June 24, 2008

Ajali ya Fung Wah Bus mjini New York

Fung Wah Bus mjini New York, Canal St. ikipakia abiria
Ajali ya Fung Wah Bus 6-23-08 Mjini New York

Wadau wanaosafiri kati ya New York City na Boston wanapenda sana kusafiri na mabasi ya waChina. Bei zao ni nafuu sana. Dola $15 kwenda, dola $15 kurudi. Si mbaya ukilinganisha na Greyhound wanaotaka dola $44 kwenda, na hiyo kurudi.

Mabasi ya waChina yanayopendwa na kujulikana sana ni Lucky Star na Fung Wah Bus. Greyhound na vyombo vya haabri walijaribu sana kuua biashara zao na walikuwa wanasumbuliwa sana na ma state troopers (polisi). Lakini waChina hawakukata tamaa na biashara yao ilizidi kukuwa. Walianza kwa nauli dola $10. Watu walidhani ni utani, lakini habari zilienea na Fung Wah Bus ilikuwa.

Greyhound walilia, maana watu waliunga mkono waChina na kuandamana walipotaka Fung Wah bus kusimamisha huduma ya bei nafuu. Sasa inabidi haya mabasi yaondoke kwenye kituo kikuu cha mabasi ya Boston, South Station. Greyhound sasa wamepunguza nauli kwenye baadhi ya mabasi yao kwenda New York City. Ndo ubepari huo.

Lakini njama ya kuua biashara ya mabasi ya waChina bado upo. Kila wakipata ajali wanasemwa. Wanaonya watu wasipande hayo mabasi ya waChina. Lakini watu bado wanapanda.

Jana huko New York, basi la Fung Wah iligongwa na lori ikiwa inapakia abiria. Mama moja aliyekuwa anavuka barabara alikufa. Ingawa si kosa la Fung Wah bus, utadhani ni kosa lao. Kwenye taarifa ya habari wanaonyesha ajali za nyuma za Fung Wah bus. Duh! Kweli njama za kuua biashara ya Fung Wah bus bado upo.

Lakini hata waseme nini, mimi bado ni mpenzi wa hiyo basi. Ukitaka usafiri wa haraka na wa hakika na ya bei nafuu kati ya New York na Boston ni hiyo! Greyhound mlie tu!

Kwa habari zaidi someni:


5 comments:

Anonymous said...

Mimi napenda sana hayao mabasi ya machina. Bei poa kabisa! Tena unafika on taimu kabisa. Kabla sijagungundua haya mabasi ilibidi nisevu ili nipande hiyo Greyhound! Tena siku hizi yako mabasi ya machina DC - New York.

Anonymous said...

Damn! Inatisha. Mimi maskini hapa USA napata minimum wage hilo ni basi langu!

Anonymous said...

i tell u ubaguzi huu jameni hayo greyhound ni mabaya afazalii hata dar express zetu za hapa bongo

Anonymous said...

Ubaguzi na uhani wa kibiashara mbaya sana isije ikawa kuna mkono wa hao greyhound katka hiyo ajali. Chemi kuna distance gani kati ya New york na Boston au inachukua mda gani kwa basi?

Chemi Che-Mponda said...

Boston- New York ni kama masaa manne au matano, hata matatu na nusu inategemeanana na trafiki.