Wednesday, April 16, 2008

Familia ya Wamisionari waponea chupuchupu - Ajali ya Ndege

Mosier Family

Kuna habari kuwa familia ya wamisionari kutoka Minnesota wamenusurika kifo katika ajali ya ndege iliyotokea jana huko Congo.

Familia hiyo ni wamisionari wa Seventh Day Adventist (waSabato) huko Iringa. Walikuwa Congo kumtembelea mtoto wao ambaye ni misionari Congo. Wanaitwa Mosier family.

Habari zinasema kuwa binti wao mwenye miaka 14 ambaye anaongea kiswahili vizuri alisaidia kupata watu wa kuokoa familia yake.

Familia hiyo inasema kuwa wanamshukuru Mungu kuwa wote walitoka na hai kwenye hiyo ajali. Wanasema kuwa ni ishara kuwa Mungu ana kazi maalum ambayo anataka wafanye.

Kwa sasa wanasema watu 36 waliokuwa ndani ya ndege walikufa, na watu zaidi ya 100 waliumia.
Ndege ilianguka kwenye soko nje ya uwanja wa ndege ya Goma huko Congo.

Kusoma habari kamili bofya:

6 comments:

Anonymous said...

Kweli Mungu yu mwema! Mungu awabariki wote walioponea kifo katika ajali hiyo. Pia Mungu alaze roho za waliopoteza aisha yao mahala pema mbinguni. Amen.

Anonymous said...

God is great,hawa watakuwa ni wamishionari wa kibidula iringa,wanakochapa vitabu na majarida yahusuyo mafundisho ya biblia.yanayomilikiwa na waadventista wasabato.
by msabato mwenzenu

Anonymous said...

Anon April 17, 2008 4:57 AM, ni mbaguzi na mdini sana, hapa hatuongelei usabato, ni ubinadamu. Ina maana umeridhika na waliokufa sio? Soma kwa makini comment ya kwanza na uisome upya comment yako, ni ya kibaguzi. Ndio maana kila siku mnalalamikiwa na ubaguzi wenu kama ulivyo fanya. Kitu kinasomwa na mamilioni ya watu unashindwa ku edit! Huna maana kabisa.

Anonymous said...

anon april 17,2008 8:10am,wewe umetafsiri ndivyo sivyo mimi nilichosema God is great ndo ilikuwa point yangu kwa hii habari,sasa nashangaa unasema mara mdini mara mbaguzi,wewe utakuwa na sababu zako binafsi.mimi wala sio mdini kama unavyofikiria.umenishangaza sana eti ndo maana tunalalamikiwa na ubaguzi wetu, kwa lipi?huo ni mtazamo wako na wala sipendi kuongelea maswala ya dini kila mtu aamini anachojua.samahani kama umekwazika.

Anonymous said...

moashe huyo mbaguzi kwahiyo wasabato hua hawafi?wewe vipi mbaguzi april 8:10

Anonymous said...

Anon April 17, 2008 10:40 PM
wasi wasi wangu ni pale uliposhukuru Mungu kwa kupona wale Wasabato, well and good, lakini kumbuka katika ile ndege walikufa watu wengine, mbona kama mtu mzima na mtu wa Mungu hukutoa pole wala kushukuru Mungu kama anon wa kwanza, na mwisho kabisa ukajitambulisha kama "by msabato mwenzenu". Bado mimi nina wasi wasi sana na hali yako ya UDINI. Nimekushauri usome comment ya kwanza na uone ujumbe na usome yako. Pole sana kama hutalijua kosa lako