Wednesday, April 30, 2008

Gary Dourdan akamatwa na madawa ya Kulevya!

Gary Dourdan
Gary Dourdan Mugshot

Mcheza sinema, Gary Dourdan (41) amekamatwa na madawa ya kulevya ya aina mbalimbali huko Palm Springs, California. Polisi wanasema alikuwa amelewa vibaya shauri ya kutumia hayo madawa na alikuwa hajijui walivyomkamata.

Kwa kweli huko Hollywood habari hizi ni za kawaida ila huyo Gary anacheza kama mpelelezi, Warrick Brown, ambaye kazi yake ni kukamata wahalifu kwenye TV Show, CSI:Crime Scene Investigation! Ni aibu kubwa sana kwake. Watu walikuwa wanamheshimu sana na alikuwa anaalikwa sehemu nyingi kuongea na vijana kuhusu jinsi ya kuishi maisha safi bila kuingia kwenye nyayo za uhalifu.

Polisi wanasema walimkuta amelala ndani ya gari, taa inawaka ndani ya gari, na gari ilikuwa upande wa barabara isiyotakiwa. Walimkuta na madawa ya kulevya mbalimbali kama unga, heroin, vidonge na mengineyo.

Kwa habari zaidi someni:


No comments: