Saturday, April 05, 2008

Yametokea Kweli!

Na Yona Maro

Ni usiku wa saa 6 nimetoka katika pilika>za maisha za kila siku , gari linasimama katika mataa ya magomeni mapipa , ghafla watoto wadogo zaidi ya 5 wanakuja upande wa dereva kama vile wanahitaji sana msaada , dereva amefunga kioo , mimi>namwangalia dereva kumuuliza kunani

Nilipokuwa namwangalia dereva upande wangu watoto wengi zaidi ya 3 wakaja wakawa wanajaribu kufungua>mlango wa upande wangu lakini ulikuwa umelokiwa wakashindwa kufanya hivyo . Gari lilivyoondoka kumbe kulikuwa na mtoto mwingine nae anajaribu kufungua mlango wa nyuma kabisa wa gari lile , gafla akaachia buti likajifunga mwingine akachukuwa jiwe na kurushia gari lile , kioo cha mlango wa nyuma kilivunjika .

Kumbuka ukipita mchana eneo hili huoni watoto hawa , ni vijana tu wanaouza maji , magazeti na bidhaa zingine hawa vijana wakienda kupumzika sasa ndio watoto wadogo wakulipwa wanaanza kuja kufanya kazi zao pia .

………………………………………………………………………………..

Saa 6 mchana nimetoka zangu mtaa wa jamhuri naenda azikiwe , nilikuwa nalamba ice cream , ghafla mtoto mmoja wa miaka kama 7 – 10 hivi akaja mbele yangu akaniomba ile ice cream nilipopiga hatua mbele zaidi akanifuata kwa mbele akitaka ile ice cream ninayolamba mimi .

Nikamsihi asininganganie sana nitampa , nikaingiza mkono mfukoni nikampatia hela nyingine lakini pale ilikuwa ni karibu na mgahawa mmoja wa chakula nikamwambia twende katika mgahawa pale nikakununulie chakula , mtoto akakataa katu akasema anataka ice cream au hela lakini hataki kwenda kula .

Nilikuwa niko katika safari zangu nikasalimu amri nikampa hela ya kwenda kununua ice cream na nyingine ya kula kwa sababu aliniahidi ataenda kula , nikapiga hatua zingine mbele nikageuka kuona anaenda wapi . Ndio mama mmoja mtu mzima akaja pale akachukuwa zile hela kutoka kwa yule mtoto , ndio maana yule mtoto akawa anataka hela kwa sababu alijua kuna mtu amemtuma .

……………………………………………………………………………….

Ukipita barabara ya ali hassan mwinyi kuelekea mwenge au mwananyamala unaweza kukutana na watoto wadogo wamebeba watoto pia , wengine wanajifanya ni watoto wao wengine wanajifanya ni watoto wa ndugu zao , siku moja nilipata nafasi ya kwenda kuongea na mmoja wao . " mambo? " "poa shikamoo ?" " marahaba ujambo "? "sijambo "?" huyo mtoto uliyembeba ni wa nani ? "ni mtoto wangu " " una uhakika ? wewe una umri gani ? "nina miaka 15 " "mtoto wako ana miaka mingapi ?" "ana mwaka mmoja karibu unusu " "niambie ukweli mbona hulingani na mtoto " "sawa , huyu mtoto ni wa yule mama aliyelala pale chini ya mti " " sasa kwanini unambebe wewe ? "

nimemkondisha kwa ajili ya kuombea hela jioni namrudisha kwa mama yake na kumpa yule mama hela kidogo ?" " huwa unapata shilingi ngapi na yule mama unampa shilingi ngapi ?" siku zingine alfu 5 au zaidi " mama huwa tunampa alfu 2 kila siku " " munampa ina maana mko wengi ?"

" ndio hao wengine nao wamekodisha hao watoto nao wanamlipa yule mama "? " yule mama amewapata wapi watoto wote hao ?" " amewatoa hospitali " " una maanisha amewaiba hospitali kutoka kwa wazazi wengine ?" " ndio hospitali ya mwananyamala "

Sintoweza kuweka maongezi mengine yaliyoendelea hapo baada ya hapo lakini ukweli ndio huo wale watoto sio wao wanakodishwa kwa ajili ya kuombea hela wengine wameibiwa katika mahospitali sasa. nashangaa wazazi wao huwa wanakuwa wapi au inakuwaje kuwaje

Yona Maro is a freelance writer and online researcher based Tanzania and frequently contributes to Tips and Topics. He has published numerous articles in local and regional publications on a wide range of topics, including Business,Ict , Education, Arts, and Local events +255 784 360204

2 comments:

Anonymous said...

du mpaka naogopa sasa nyumbani sasa hali hiyo tutakwenda kuishi bongo kweli

Anonymous said...

Huyu Yona ni muongo na tapeli. Kama si tapeli, kwa nini hajaripoti hili tukio polisi ili watoto hao wapate haki yao? Yaani yeye ameona ni hadithi nzuri tu ya kuja kuweka kwenye blog, na si kutoa taarifa polisi watoto hao waokolewe?

Nimemsikia siku nyingi sana huyu jamaa anayejiita Yona Maro, ni muongo mkubwa!