Tuesday, April 29, 2008

Sinema - Paul Blart:Mall Cop

Mimi na Mcheza sinema, Jamal Mixon kwenye set ya Mall Cop
Mimi na Mcheza sinema, Jerod Mixon


Mcheza sinema, Kevin James
Mcheza sinema, Jayma Mays
Segway

Wadau, jana nilikuwa extra kwenye sinema, Paul Blart:Mall Cop ambayo itakuwa sinema ya vichekesho (Comedy). Nilishinda kwenye seti huko Burlington Mall siku nzima. Kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa nne usiku (8:30am -10:00PM). Tulifanya kwanza scene ya arusi. Bwana arusi ni Kevin James na Bibi Arusi ni Jayma Mays. Kevin ndo mhusika mkuu wa hi sinema, yeye ndiye Paul Blart:Mall Cop.

Kwanza tulipiga scene tumekaa kwenye meza kama wageni waalikwa. Food Court ulikuwa umepambwa kama ukumbi wa arusi. Halafu walipiga scene kadhaa, wanafungishwa ndoa, busu, Bibi harusi kutupa bouquet, wahusika wakuu wengine wa sinema waki-react kwenye arusi. Halalfu walipiga scene za Bibi na Bwana arusi kuondoka wakiwa kwenye segways. Halafu tuliambiwa tucheze densi. Wimbo ulikuwa, 'Ain't No Mountain High Enough' ulikuwa unaimbwa na kaka yake Kevin James.

Mwisho walicheza densi wakiwa kwenye segways ndani ya gazebo. Hapo tuliambiwa tuzunguke gazebo. Ilitokea kichekesho wakati titi la Jayma ilitoka nje ya gauni la arusi. Watu walichecka walisema kumbe ana matiti feki. Yaani unaona kabisa ni mpira wa kupachikwa.
Basi, kuna kipindi tulikuwa tunapumzika. Akatokea mcheza sinema, Shirley Knight, ambaye anacheza kama mama yake Jayma Mays. Alikuja mezani kwetu alichukua kisu na kasema, "Naomba mtu anichome kisu!" Heh! Tulipigwa butwaa na kubakia midomo wazi. Alichukua kisu na kuanza kujichoma maeneo ya tumbo. Tukadhania huyo mama ni mwendazimu. Basi aliishia kucheka na kusema kavaa mapedi kusudi aonekana ni mnene maana siyo mnene hivyo. Hapo na sisi tulianza kucheka. Lakini kwa kweli tulishikwa na woga.

Kwenye scene ya mwisho ya arusi, mimi na mama mwingine mweusi tuliambiwa tusimame na Jamal Mixon. Nilifurahi kweli maana hapo chensi ya kuonekana vizuri kwenye sinema inakuwa kubwa kama uko na moja na wahusika wakuu wa sinema. Jamal utamkumbuka kwenye sinema kama, The Nutty Professor na Gridiron Gang.

Baada ya kumaliza scene ya arusi, tuliambiwa tubadilishe nguo. Halafu tulipiga scene ambayo tunakimbia. Jamaa anafoka, "Kuna mtu mwenye bastola!" Basi ndo tunakimbia kutoka nje ya mall. Karibu tukanyagane utadhani mtu alikuwa na bastola kweli.

Wakati tunasubiri kupiga hizo scene niliongea na Jamal na kaka yake Jerod Mixon. Kwa kweli ni vijana poa sana. Tuliongea kuhusu sinema za Hollywood na jinsi roles kwa ajili ya weusi ambazo ni za maana ni chache. Jamal alisema kuwa anatunga screenplays sasa akiwa hayuko kwenye sinema.

Kuona scene kutoka The Nutty Professor Bofya linki chini ni sinema ya kwanza ambayo Jamal alifanya wakati huyo ana miaka 14:

4 comments:

Anonymous said...

Dada Chemi kweli ulikuwa na watu wa Hollywood! Hii Kiboko! Hongera!

Anonymous said...

Hongera Da Chemi! Msalime Jamal, nampenda sana kwenye The Nutty Professor na The Klumps.

Simon Kitururu said...

Moto huohuo Da Chemi!Kila la kheri!

Anonymous said...

Mambo si ndo hayo! HONGERA SANA! Karibu itabidi uwe na Fan Club!