Thursday, April 10, 2008

Wanaume wapigwa na wake zao Bongo!


Hii story imenifurahisha mno! Equal opportunity! Kweli TAMWA imeamsha akina mama Bongo!

***********************************************************

Kutoka ippmedia.com

Spika afichua siri za wanaume wanaopewa kibano na wake zao

2008-04-10

Na Sharon Sauwa, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Samuel Sitta amewaacha hoi waheshimiwa wabunge alipotoa taarifa ya utafiti kuhusu wanaume wanaopigwa na wake zao. Baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu, Spika alieleza kuwa ana ujumbe kutoka kwa mmoja wa wabunge ambaye amemuomba kurudia taarifa yake kuhusiana na utafiti huo.

``Nimepata ujumbe hapa tena kutoka kwa mheshimiwa mwanamke ambaye ananiomba nirudie kutamka kuhusiana na utafiti,``akasema. Spika alisema utafiti unaonyesha asilimia 35 ya wanaume wanapigwa na wake zao ingawa hawasemi kutokana na kuona aibu.

Akasema hata kesi za namna hiyo haziripotiwi polisi kutokana na akina baba hao kuogopa kuchekwa. Akasema asilimia hiyo inajumuisha pia waheshimiwa wabunge wanaume wanaokandamizwa makonde na wake zao.

5 comments:

Anonymous said...

Ha ha ha Da Chemi, it is nothing coz sisi wanaume tunajuwa kwamba "kofi la mpenzi haliumi". In real sense mwanamke anaepiga ni yule mwenye mapenzi ya kweli kwa mumewe au mpenzi wake, lakini bahati mbaya mume huyo au mpenzi wake huyo amemtenda sivyo ndo anaamuwa kumrudi, kwa hiyo wanaume hao hawaoni sababu ya kushtak sababu inakuwa nikweli walitenda makosa hawakupigwa kwa kuonewa!
Da Chemi mimi naamini wivu ndio mapenzi kama mwananume atakaepigwa na mkewe kwa wivu basi ashkuru sana, coz anapendwa simchezo, mwanamke kama hakupenda hana muda wakukupiga, kwa lipi?! Na kwanini agombane na mtu asompenda? simply atachukuwa time yake au nayeye atalipiza kama wewe ulitembea nje na yeye atatembea kazi kwisha!

Anonymous said...

Da chenmi unafurahia hiyo picha wakati mwenzio kapigwa karibia na...na huyu dada sijui vipi akimpasua mwenzie je?

Anonymous said...

HATA HIVYO NI WACHACHE SANA WANAOPIGA WAUME ZAO,WANAWAKE WENGI NI WAOGA SANA.

Anonymous said...

Hii bongo kama ni Dsm tu naweza kubali, bali kama ni Tanzania nina walakini na representativeness of the sample size.... IMO, it's too generalized naona... Labda kama ni kupigwa kwingine...

Anonymous said...

Duh ! hicho kifuti cha katikati ya maungio ya uzazi kimenoga kweli
kuna mtu alimwomba mungu hivi
"Dear Lord,
I pray for Wisdom to understand my man; Love to forgive him; And Patience for his moods. Because, Lord, if I pray for Strength, I'll beat him to death.
AMEN
Kwa hiyo hiyo ni rasha rasha bado za masika hazija mnyea