Monday, April 21, 2008

Kitanzini Iringa


Kuna baadhi yenu mliotaka kujua zaidi ya kihistoria kuhusu Kitanzini, Iringa. Pichani Mzee Nzowa bado anakumbuka mahala hasa uliposimama mti uliotumika na Wajerumani kuwanyongea Wahehe. Mahala hapo palijulikana kama Kitanzini.
Aliyefikishwa hapo alifungwa kitanzi shingoni na kuning'inizwa hadi kifo. Utotoni Mzee Nzowa alikua akiuona mti huo ingawa watu hawakuendelea kunyongwa hapo baada ya Mwingereza kuingia nchini.
Mti huo wa kihistoria anadhani ulikatwa miaka ya 50 wakati wa kutengeneza barabara za mitaa. Hadi hii leo eneo hili linajulikana kama Kitanzini. Kwenye nchi za wenzetu wangeweka haraka mnara wa kumbukumbu ili kuitunza historia kwa vizazi vijavyo.

9 comments:

Anonymous said...

Bora wazee kama hao wapo kutukumbusha historia yetu.

Anonymous said...

we kazi kukopi tu vya wenzio

Anonymous said...

If you can't beat them, then copy them, Huajfanya jambo la ajasbu ndugu yangu. Mimi ninachojua Dada Chemi huwa anajitahidi kutuletea various of intersting news(according to her touch!!) ambapo imetusaidia sana sisi tusioweza (kwa kukosa muda) kutembelea blog zote.(Sitaki kumsemea Da Chemi anyway).

Kwa Hiyo Historia ni muhimu kwa kila mtu kuieneza hata kama ikikopiwa mara kwa maelfu.

Mimi nimeishi mji Huo Utotoni, Kinachonishangaza miji yetu bado haijaweza Kuplot vivutio vya Kitalii hasa hivi vya Kihistoria. Wanadhani Utalii mpaka Uende Mbugani.

Hili ni jukumu la kila Mmoja. Mimi Binafsi nina Mpango wa kufungua Blog (very Soon) itakyojikita katika kuelezea vivutio vya Kihistoria ambavyo havifahamiki au vinapuuzwa kwa namna moja au nyingine Nchini(Tz).

Stay Tuned

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 12:56am, ni jambo la kawaida ku-copy kitu kutoka blog ya mtu mwingine. Mradi unatoa 'credit' ulipoitoa hakuna neno. Ila kuna bloggers wengine hawa fuati hiyo 'etiquette' ya crediting. HJapo mambo yanakuwa mabaya.

Anonymous said...

Anon April 22, 2008 12:56 AM
unamsakama huyu dada wa watu hana maneno, nenda kule kwa akina nanihiii ukaambiwe unachafua hali ya hewa. Mtu mshari kama nini! Sasa alivyokujibu kistaarabu sijui unajisikiaje. Acha hizo ndugu!

Anonymous said...

nyie mnaomsemea ni kama nani/mnapenda kujipendekeza mi nilikua namwambia ninachokiona coz kila siku mi natembelea blog zote na nakkuta vitu vinalingana,na huyu shosti anasema ooh mara kutoka kwa mjengwa,mara ohh kutoka kwa michuzi na sijamtukana nimemwandikia kwa ufupi sana..na hata huko kwa kina nanihii mbona sana tu nachafuaga hali ya hewa hilo usiulize

Anonymous said...

Una roho ngumu wewe! Haya kaka/dada

Anonymous said...

mi siyo mnafiki ndomana naroho ngumu,nimemwambia na kanielewa nayeye kanielewesha tatizo lipo kwenu wapambe nuksi

Anonymous said...

No good grain no good coments it's always work like that