Saturday, April 19, 2008

Moto Shule ya Boarding UgandaHuko Afrika ni kawaida kupeleka watoto boarding (shule ya kulala) ili wapate elimu. Huko Uganda wiki hii watoto wa kike 19 walipoteza maisha yao baada ya bweni lao kuchomwa moto. Polisi Uganda wanasema kuwa moto uliwashwa maksudi (Arson). Bweni hiyo ya shule ya msingi Budo, ilikuwa inalaza wasichana 58.

Aende motoni huyo aliyewaua hao mabinti!!! Walikuwa nio watoto wa shule ya msingi wenye miaka 9 hadi 12 tu. Kwa kweli kuna watu wenye roho ya kutu katika dunia hii. Sijui walimkosea nini huyo aliyeamua kuwaua!

Kwa sasa polisi Uganda wameshilikia walinzi tisa wa shule na matron.

**********************************

4-19-08

(AP) Ten people being held in connection with a fire that killed 19 Ugandan schoolgirls are all school employees, a senior police official said Saturday.

Nine guards and a matron are being held on suspicion of negligence, said the officer, who asked for anonymity because he was not authorized to comment on an ongoing investigation.

The officer said police suspect that Monday's fire at Budo junior school was started by arsonists. Witnesses reported a loud bang as the building burst into flames. The doors to the dormitory had been locked from outside.

Young survivors spoke of struggling to climb through tiny windows as their sleeping quarters filled with smoke.

Police are following two leads involving disgruntled school staff, the officer said. They have offered $3,000 for information.

The fire was the third fatal school fire in Uganda in two years.

4 comments:

Anonymous said...

DUH! Hiyo story inasikitisha. Mungu awalaze mahali pema mbinguni. AMEN.

Sasa wanadhani hao walinzi wote na matron walihusika?

Anonymous said...

Ah Da Chemi waulizia sababu za muuaji kufanya hivyo...! Fatma Issa aliimba kwenye wimbo wake mmoja wazamani kidogo anasema hivi".. tahadhari na adui kiumbe,daima asikusibu mungu akuepushie, huyo si mzuri, simzuri hata chembe, wala hataki sababu adhabu akutie.."
Kwa hiyo Da Chemi hasidi hana sababu!
Lakini akaendelea tena kuimba Fatma issa akisema "...heri adui shetani, kama adui kiumbe, malipo ni duniani akhera kwenda hesabu.."
Kwa hiyo na yeye atalipwa hapa hapa duniani!

Anonymous said...

Hao watoto walimkosea nini masikini ya Mungu malaika wadogo wasiojua chochote duniani? Lakimi Mungu Mkubwa huyo adhabu yake ataipata hapa hapa duniani maana hakuna nafsi ya mtu inayopotea bure. Mungu amlani huko aliko na kila siku iendayo kwa Mungu iwe ni adhabu kwake, kila alifanyalo silifanikiwe, na maisha yake yawe na madhila hata kama atajificha wapi!

Anonymous said...

jamani Da Chemi!! walichoma makusudi!! Toba dunia imekwisha, unawezeje kuwa na kisasi na watoto wadogo hivi. Ehe Mungu utuhurumie loh!