Wednesday, April 23, 2008

Sinema - This Side of the Truth

Ricky Gervais akidirect scene. Leo alikuwa amevaa nguo hizo hizo, nadhani ana suruali 20 and sharti 20 za aina moja.
Nguo nilizovaa kwenye scene.
Hii ni sehemu ya seti. Hapo eti ni theatre inaonyesha sinema ya chanzo cha magari. Hebu tazama vizuri...hiyo siyo sinema hall ni benki. Ila set designers wameipamba kusudi ionekane kama sinema hall kwa nje.
Hapa crew wanafungasha kusudi waende zao nyumbani.

Leo nilikuwa extra kwenye sinema, THIS SIDE OF THE TRUTH. Stelingi wake ni mwingereza Ricky Gervais. Inapigwa Lowell, Massachusetts na Andover, Massachusetts. Tulikuwa Downtown Lowell, kwenye benki.

Crew wake wengi wanatoka Uingereza. Basi ilikuwa kichekesho watu walikuwa wanalalamika kuwa wanshindwa kuwaelewa wakiongea. Kweli kama umezoeza kiMarekani, kusikia Kiingereza halisi ni shida. Nilikuwa nawatafsiriwa wazungu niliokuwa nao. Wanauliza kasema nini? Nami najibu kasema hivi, na wao wanasema "Oh!". Nami nikasema huenda na sisitukiongea anapatashida kutuelewa.
Picha chache hizi kutoka seti. Haturuhusiwi kupiga picha kwenye seti. Hizi nilipiga baada ya kumaliza shoot. Leo nilikuwa mpita njia, natembea nyuma ya Ricky Gervais. Lakini hasa walitumia gari yangu. Walibadilisha plates. Nikatoka holding (wanapopumzika extras) na kwenda kwenye seti, sikutambua gari yangu mpaka niliona permits zangu kwenye dirisha.

Wanasema wataniita tena. Wiki ijayo nitakuwa kwenye sinema, Mall Cop tena.

12 comments:

Subi Nukta said...

Kazi njema!
Ufanikiwe!

Anonymous said...

Chemi,I wish you would be born again,become teens,yu would made great in industry.You hardworker baby,keep it,go baby.Never know when yu mighty bea Star!

Unknown said...

hmm... poa hiyo filamu itakamilishwa na kutolewa lini?

nakutumia salamu kutoka huku new york
mbu
(mkenya fulani anaoishi ng'ambo)
:-)

Anonymous said...

well done chemi may god bless you uzidikufanikiwe
mdau

Anonymous said...

Sasa dada chemi wewe kiingereza halisi umejifunza wapi? maana hata mimi nilipofika Uingereza siku ya kwanza nilikuwa nasikia kwikwi tuu waingereza wakiongea. Siku hizi (baada ya miaka 9) ndo kidogo naanza kuwaelewa.

Anonymous said...

Dada me napenda kujua ukiwa extra kama hivyo huwa unalipwa?na hiyo malipo inarange kwenye kiasi gani?

Mrisho's Photography said...

Kwa faida ya mastaa wetu wa Bongo, Extra ndo nafasi ipi kwenye muvi?

Chemi Che-Mponda said...

Extras ni actors wanacheza nyuma ya lead actor (mhusika mkuu) kusudi scene ionekana kama ni jambo ambayo inatokea kweli. Mfano kama ungeona actors wanacheza peke yao bila watu wengine mgeona ni kitu cha ajabu. Hivyo ukiona actor anaenda supermarket, ni lazima kuna watu wengine mle, basi extras tunajifanya shoppers, wahudumu etc. Actor kasimama kwenye foleni, hasimami peke yake lazima kutakuwa na watu wengine, basi zinajazwa na extras. Ukiona actor anakwenda ofisini lazima kuna kuna na watu mle, basi ndo kazi ya extras.

Pia kuna mdau ameuliza jinsi ya kuwa Extra. Kwanza piga headshot. Hiyo ni kama business card ya actor. Halafu u-sign na casting agency. Hapa Boston tuna Boston Casting, CP Casting, LDI Casting, na Maura Tighe Casting.

Anonymous said...

Hongera sana Da' Chemi. Nakuombea mafanikio katika hii safari ambayo umeanza mbali. Penye nia pana njia.

Anonymous said...

Hongera kwa kazi nzuri,keep it up Dada. Harafu ulipendeza!

Mrisho's Photography said...

asante dada Chemi kwa jibu lako zuri, kwani hapa kwetu ma producer na ma director wetu huwaonesha watu kwenye sinema zao bila makubaliano yoyote na hata mtu akijiona kwenye sinema ambayo hakuulizwa wala kuombwa ridhaa haoni kama ametendwa sivyo, yumkini ataona fahari, wakati kumbe hiyo ni dili wenzetu wanalipwa! Sisi bado!

Chemi Che-Mponda said...

Mrisho,

Kwa kweli hapo umegusa pointi ya maana. Hapa Marekani kila mtu ambaye unamwona kwenye sinema kasaini release. Kama hasaini basi hiyo sehemu haitoki kwenye sinema. Ni sheria. Pia hao watengeneza sinema wanaweza kuwa sued. Hivyo ukiona sinema, ujue kila mtu mle ambaye unaweza kuona uso wake ni actor.

Hata kwenye taarifa ya habari kama hujasaini release hawawezi kukuonyesha. Au wanaweka blur kwenye uso wako. Ila kwenye news hulipwi.