Wednesday, April 09, 2008

Ninaomba msaada jinsi ya kupambana na tatizo hili - Subi

Kutoka kwa mdau Subi:

Waheshimiwa,

Naomba msaada wengu kwani kuficha haya maradhi sasa imefika mwisho, yanaumbua, wahenga walishaonya.

Ninajua mpo watu mtakaosema tulizembea kumlea ndugu yetu ama hatujui malezi, mtatushurutisha kuwa tumelikoroga basi na tulinywe, mimi nakubali yote, rusheni mawe, pigeni vijembe, malizeni matusi na kejeli zote, lakini ukweli unabakia pale pale, hili halinyweki!
Mimi ndiyo hivyo tena maji nshayavulia nguo, kuyaoga sina budi. Tafadhali rejezeni roho zenu za huruma, ninakuombeni ushauri.

Shida yangu hii:

Ninaye ndugu aliyekumbwa na tatizo la utumiaji madawa ya kulevya.
Juhudi binafsi tulizoafanya hadi sasa ni kumfanyia sala, dua na maombi, pamoja na kumfikisha ndugu yetu huyu katika hospitali mbalimbali kwa matibabu zaidi. Hospitali na vituo tulivyovitumia ni pamoja na: Mawenzi Hospitali Moshi, KCMC Hospitali Moshi, Mirembe Hospitali Dodoma na Lutindi Hospitali Tanga.

Tatizo hili limemvuruga yeye, sasa hasikizi suala la mhadhini wala la mteka maji kisimani. Sasa wanandugu tunavurugana na kuchukizana.

Ndiyo maana ninaomba ushauri kutoka kwenu.

Ikiwa umewahi kukumbwa na mkasa kama huu, Je, ni hatua gani ume/mnachukua kumsaidia ndugu yenu huyo?

Ikiwa hujakumbwa na mkasa kama huu, Je, unao ufahamu wowote wa jinsi ya kuwasaidia wanaoathirika kutokana na vitendo vya muathirika ili waweze kuchukuliana na tatizo hilo?

Je, unafahamu kituo chochote nchini Tanzania ambacho kinashughulika na watu walioathirika na madawa ya kulevya?

Natanguliza shukrani za dhati!

3 comments:

Sophie B. said...

Pole kwa tatizo hilo,jaribu sehemu hizi Dar es Salaam

SOBER Tanzania
P.O. Box 10713
Dar es Salaam
Tel: 022-2118616

AMREF
P.O.Box 2773
Dar es Salaam
Tel: 022-2116610
Fax: 022-2115823
Email: amreftz@africaonline.co.tz

Department of Psychiatry
P.O. Box 65023
Dar es Salaam
Tel: 022-2152723

Save the Children
P.O. Box 10414
Dar es Salaam
Tel: 022-2760798
Email: scfdar@maf.org.uk

and keep praying for him/her-
Dada S
http://absolutelyawesomethings.blogspot.com/

Subi said...

Ndugu ©absolutelyawesomethings

Ninashukuru sana kwa anwani na mawasiliano ya vituo ulivyonipatia.
Shukrani kwa moyo wako wa huruma.

Anonymous said...

Usijali nakuombea mafanikio.