Thursday, April 03, 2008

Ufisadi na Uchawi

Imeandikwa na mdau SUBI.

The Land of Kilimanjaro, Olduvai, Serengeti, Tanganyika, Zanzibar, Ufisadi and Uchawi!.... of course there are exceptions! Na ndiyo ukweli wenyewe kwa baadhi ya WaTz.Wametusema sawasawa.Nchi ya wachawi? Na ndiyo maana bado tunabishana kuhusu nani ameficha kiatu cha kukimbilia, wakati wenzetu wameshajipanga kwenye mstari.

Na tukishakipata kiatu cha pili tunacholitafuta, kiatu cha kwanza watakuwa wajinga fulani fulani wanaojiona werevu sana wamekificha ama wamekitoboa. Yaani ali munradi tuna visingizio gunia tele.Kazi tumekalia kusema na kuamini uchawi, uvivu, kusemana, kutafutana visa, kuomba omba na kuamini miujiza tuuuuuu badala ya kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa.

Yaani mtu anaamini kabisa kuwa atapataga mautajiri ya fasta fasta kwa ulozi. Hata anayejitahidi kufanya kazi anaogopa kutishwa kulogwa. Yaani ni aibu mfanowe hakuna.Dawa? Elimu inayoendana na wakati na mazingira. We mtu anafundishwa nadharia tu shuleni, vipindi vya vitendo, maabara hamna vifaa ya kutosha ama hakuna kabisa vifaa, anaishia kukariri tu, sasa huyu mtu akihitimu atatarajiwa vipi afanye kazi kwa ufanisi?

Ndiyo usanii tena unakuja bila kutaka. Maneno meeengi, kuagiza kwiiingi, lakini mwambie akuonyeshe kwa mfano kwa vitendo..... utasikia, 'fanya tuu', 'yaani hujui', 'hiyo rahisi', Ningejua ningeuliza? Shule ndiyo zimeshakuwa sehemu za kukulia tu sasa na kujifunza ujamaa! Maanake walimu wanasema utajifunza utapoanza kazi!Wengine wenu mtanichukia tu lakini ndiyo hivyo tena, nimeshayasema mawazo yangu, kwani nimekulazimisha ukubali? Hatufanani!

Subi (usibofye jina langu)'

Witchdoctor killings condemned

NAIROBI (Reuters) - Tanzania's President Jakaya Kikwete has condemned witchdoctors who kill albinos and harvest their body parts in the hope it will bring prosperity.

He said 19 albinos had been murdered since March 2007, and another two were missing presumed dead in the east African country.

"Sometimes, word spreads around that body parts of people with certain physical attributes like bald people or albinos contribute greatly to attaining quick prosperity," Kikwete said in a monthly state of the nation speech late on Wednesday.

"These killings are shameful and distressing to our society," he added.
Albinos are often accused in Tanzania of being witches themselves.

There are an estimated 270,000 people who suffer from the condition which stops them producing pigment in their skin, hair and eyes in the country of 39 million.

Kikwete blamed charlatan witchdoctors, many masquerading as traditional healers, for extracting body parts such as genitals, tongues and breasts.

"Many of the witchcraft killings happen because of a false belief that by using other peoples' body parts they can succeed in business or in activities like mining or fishing," Kikwete said.
Most killings took place in the Victoria region and were committed by gangs for hire, he said.
(Reporting by George Obulutsa; Editing by Giles Elgood)

1 comment:

Anonymous said...

Safari za Bagamoyo haziishi!