Thursday, April 24, 2008

Wesley Snipes Ahukumiwa Kifungo - Miaka Mitatu!


Jamani, leo nimejua ubaguzi bado upo nchi hii. Wesley Snipes amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwenye gereza la serikali (federal). Kisa hakulipa kodi aliyostahili kulipa! Denzel Washington alikuwa mahakamani akitoa shuhuda kuhusu jinsi Snipes alivyo mtu mwema. Pia Woody Harrelson alitoa shuhuda. Snipes mwenyewe alimwomba hakimu amwonee huruma! Lakini wapi! Jaji kampa kifungo cha juu kabisa miaka mitatu. Alisema awe mfano kwa wengine!

Ninaamini angekuwa mzungu kama Tom Hanks au Tom Cruise angepewa probation, au kifungo cha siku chache au miezi michache.
Marekani lazime ulipe kodi. Kama hulipi utakamatwa tu. Kama si leo basi hata baada ya miaka!

Wadau mnasemaje?
Kwa habari zaidi someni:

6 comments:

Anonymous said...

ndo muondoke kwa watu nawewe unalipa kodi?siyo mnalalamika tu

Anonymous said...

he reaped what he sowed,how come someone from humble begginings.make such a mistake,greed,greed,greed,greed,greed and not being gratefull have now put him in his rightful place. i hope on appeal wamuongezee miaka

Anonymous said...

"Jamani, leo nimejua ubaguzi bado upo nchi hii" What makes you say that? Kama unaishi America, advice you will hear from everywhere is "DO NOT PLAY WITH IRS". Besides! Where did you get this news kwamba Denzel alikuwa mahakamani akitoa ushuhuda? Please STOP MISLEADING. Anywayz, You will be execused kama bado kiingilishi kinapinda. Also stop being opinionistic. Just bring news, usianze kupotosha ukweli kwa ukalimani usio na maana. Please read this piece below from CNN and then compare with your kiingilishi. TOTALY GOIN' DIFFERENT DIRECTIONS.

Actors Denzel Washington and Woody Harrelson, as well as television judges Joe Brown and Greg Mathis, submitted letters to the judge on Snipes' behalf.

In his letter, Washington said Snipes was "like a tree -- a mighty oak ... Many who know him have witnessed the fruit of his labors, have sat in his shade and even been protected by his presence. I am proud of him, proud to call him a fellow thespian and most importantly, proud to call him a friend."

Anonymous said...

Kwa miaka lukuki uliyoishi USA inashangaza kusema kuwa eti ndo umejua kuwa kuna ubaguzi! Ni Amerika ipi unayoishi ambapo hakuna ubaguzi? Hata hivyo, suala la kutolipa kodi halina mjadala. Kama huyo jamaa angekuwa kapakaziwa hapo ungekuwa na haki ya kulalamika. Hivyo, kama ushahidi upo kuwa hakulipa, wacha sheria ifuate mkondo wake.

Anonymous said...

UBAGZUI UPO SANA TU USA! HAITAISHA!

Anonymous said...

Kwanza kabisa mimi si mpenzi wa Sinema na pia si mshabiki wa Wesley Snipe, lakini namuhurumia kwa msukosuko huo.

Tukiliangalia suala hili katika jicho lingine, kwanini mtu millionea kama Wesley Snipes akwepe kulipa kodi? (Kama ni kweli hakuwa akilipa kodi) Au ndo matatizo ya kukosa "Class" na kutoka katika u-machafuchafu basi hata ukijaaliwa kuachana na u-machafuchafu bado utaurudia tuu?

Huyu siyo mtu wa kwenda jela kwa kosa kama hili.