Thursday, April 24, 2008

Mchele umekuwa Adimu Marekani!


LOH! Haya sasa ni makubwa! Mchele umekuwa adimu Marekani, mpaka maduka yana weka 'limit' ya kiasi ambacho unaweza kununua. Nilikuwa nimesika fununu wiki iliyopita lakini sikutaka kuamini.

Mchele hasa ambao sasa umekuwa haba ni zile Basmati (pishori) na Jasmine (ya kunukia). Sehemu zenye wahindi wengi ndo wanaumia. Hebu fikiria watu wapenda madishi ya wali kama sisi waafrika na wahindi tukianza kukosa! Si itakuwa balaa! haya tuanze kuzoea pasta (spaghetti). Utakuwa kama enzi za mwalimu na miezi 18 (miaka 18). Sidhani kama hali unaweza kuwa mbaya kiasi hicho lakini.

Kwa kweli ni jambo la kushangaza sana kusikia uhaba wa chakula. Hata hivyo ni watu ambao wali ni chakula chao kikuu ndo wanaanza kuona uchungu. Bei umepanda mno. Hata hivyo bei ya vyakula kwa ujumla umepanda.

Yaani nikienda supermarket siku hizi nasikia hata wazungu wanalamika kuhusu bei ya chakula. Bei ya cereals, mikate, mayai, maziwa, nyama umepanda. Pia bei ya petroli umepanda mno . Na mimi nasema ukisikia mzungu analalamika basi unajua kweli hali umekuwa mbaya!

Hayo matatizo ni Asante Bush na vita yake isiyo na maana!

Naomba Obama achaguliwe kuwa raisi!

**********************************************************

Skyrocketing rice prices has Sam's Club limiting sales
4-24-08

(CNN) -- Retail chain Sam's Club will limit the sale of large quantities of rice amid a dramatic increase in the global price of rice.

Sam's Club will limit customers to four 20-lb. bags of jasmine, basmati and long-grain white rice.

The store will limit customers to four 20-lb. bags of jasmine, basmati and long-grain white rice, the company said in a statement. Its restriction mainly will affect businesses that buy rice in bulk, but the company said "a typical Sam's Club Business Member does not buy more than 80 pounds of rice in one visit."

"We currently have plenty of rice for Sam's Club members," the statement said. "This temporary restriction does not apply to retail-sized rice for sale in Sam's or elsewhere at Wal-Mart stores."

The restriction does not apply in Idaho and New Mexico.

Sam's Club -- a division of Wal-Mart Stores Inc. -- has 593 wholesale locations in the United States and more than 100 abroad, in countries such as Brazil, Canada, China and Mexico.
Food prices have soared worldwide in recent months, leading to violence in some developing countries.

"In just two months," World Bank President Robert Zoellick said this month, "rice prices have skyrocketed to near historical levels, rising by around 75 percent globally and more in some markets, with more likely to come."

4 comments:

Anonymous said...

Dada Chemi, nina wasiwasi kuishi "unyamwezini" kunaanza kuathiri kiswahili chako! Wewe ukiwa mwandishi ningetarajia uandike kwa kutumia lugha fasaha. Hebu soma tena ulichoandika!

[Sidhani kama hali unaweza kuwa mbaya kiasi hicho lakini.

...bei umepanda mno. Hata hivyo bei ya vyakula kwa ujumla umepanda].

Kiswahili fasaha ingekuwa (Sidhani kama hali inaweza kuwa mbaya kiasi hicho lakini.

...bei imepanda mno. Hata hivyo bei ya vyakula kwa ujumla imepanda).

Anonymous said...

nakuja marekani mwezi ujao,ngoja nijibebee mchele wangu wa kyela walau kilo 5.

Anonymous said...

Sembe, people will be starting eating sembe more often, for those who have maize farms/plantation, business is booming, forget OIL excavation, keep it for future. Get A TRACTOR not spirited JEMBE la mkulima, it doesn't work. It will pay off big time. Trust me on this.

It will be disastrous in Africa, Can we plant rice in our country??, I know people are thinking what I am thinking, massive farms buy, Wakulima be ware.

Kilimo at front page, is our government doing enough to encourage wakulima, assisting on Kilimo bora and all the theme, never mind we can be exporters of food grains one day..Keep thinking Tanzania, keep thinking.

Get rid of those sisal plantations in Tanga and other places, and start doing a right thing, Grains plantations, like Wheat, rice, Maiza and others.. Government start acting or are we waiting for inevitable until Muzungu come to advice us on the issue.

By Mchangiaji.

Anonymous said...

Nimenunua gunia la 20 pounds. Sasa nitakuwa naipima hasa. Hakuna wastage tena!